Halmashauri ya bima ya kitaifa ya matibabu, NHIF imetangaza uteuzi wa Elijah Wachira kuwa Afisa Mkuu Mtendaji na wakurugenzi wengine sita wa bodi hiyo.
Uteuzi huo ulitokana na mchakato wa wazi wa uajiri uliofanywa kupitia kwa tangazo la mitandaoni Juni 27 mwaka huu.
Wakurugenzi kwenye bodi hiyo ni Bi Hazel Koitaba, atakayesimamia hazina hiyo,Ibrahim Mohammed, atakayekuwa Mkurugenzi wa masuala ya mashirika,Pariken Ole Sankei ambaye ameteuliwa Mkurugenzi wa Ukaguzi .
Catherine Mungania, atasimamia maswala ya sheria wakati Robert Ingasira, akiteuliwa Mkurugenziwa masuala ya kifedha huku Martin Ayoo akiteuliwa Mkurugenzi wa habari mawasiliano na Teknlojia.