Jamii zinazoishi karibu na Mabwawa ya kuzalisha umeme ya Seven Forks Dams, zimetakiwa kuhamia katika nyanda za juu kuhofia mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha hapa nchini.
Maeneo yaliyo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na mafuriko hayo ni pamoja na Hola, Garissa, Garsen,
Katibu katiwa wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo, alionya kuwa bwawa la Kiambere limejaa hadi pomoni na kuna uwezekano mkubwa wa maji kuanza kutiririka.
Onyo hilo linafuatia kuongezeka kwa kasi ya maji yanayoingia kwenye mfumo wa mteremko kutoka maeneo ya vyanzo vya maji ya Mlima Kenya na Aberdare.
Kulingana na Omollo, Bwawa la Kiambere limepita kiwango chake kamili cha usambazaji, na hivyo kuongeza hatari ya mafuriko yasiyodhibitiwa chini ya mkondo.
Ili kupunguza tishio hilo, serikali imeanzisha mikakati kamili ya kukabiliana na dharura.