Madereva mashuhuri wa kampuni ya Toyota Gazoo, Oliver Solberg, Sebastien Ogier na Elfyn Evans, wamelazimika kujiondoa mashindanoni Jumamosi baada ya magari yao kukumbwa na hitilafu.
Baada ya vituo 13 vya mashindano hayo yanayoendelea mjini Naivasha, tayari madereva Jumamosi wamekabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo kufutiliwa mbali kwa kituo cha Camp Moran 2 baada ya kuharibika kwa barabara kutokana na mvua kubwa.
Kujiondoa kwa wawili hao kunamwacha Katsuta Takamoto akiongoza kuelekea katika mzunguko wa jioni Jumamosi.
Karan Patel, akiendesha gari aina ya Skoda Fabia, ndiye dereva bora kutoka Kenya, akishikilia nafasi ya 19, akifuatwa na Aakif Virani aliye wa 22 huku Samman Vohra akiwa wa 25.