Uwanja mdogo wa ndege ulio katika mbuga ya kitaifaya wanyamapori wa Amboseli umefungwa kwa muda baada ya kuathiriwa na mafuriko.
Kwa kawaida watalii hupaa kwa ndege kutoka uwanja wa Wilson hadi mbuga hiyo ya Amboseli.
Uwanja huo umelowa maji kutokana na mvua ambayo imekuwa ikishuhudiwa tangu wiki jana.
Shirika la wanyamapori KWS limeahidi kuufungua tena uwanja huo hivi karibuni kwa matumizi.