Upinzani waandamana DRC kupinga marekebisho ya katiba

Upinzani unashinikiza kuondolewa kwa mswada wa kura ya maoni unaosubiri kusomwa kwa mara ya pili bungeni.

Tom Mathinji
1 Min Read
Upinzani waandamana DRC kupinga nyongeza ya muhula wa kuhudumu wa Rais.

Mamia ya waandamanaji walikusanyika katika Jiji Kuu Kinshasa, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupinga kile walichokitaja marekebisho ya katiba kumpa fursa Rais Felix Tshisekedi kuwania muhula wa watu uongozini.

Upinzani unashinikiza kuondolewa kwa mswada wa kura ya maoni unaosubiri kusomwa kwa mara ya pili bungeni, ukionya dhidi ya hatua yoyote ya kuongeza muda wa urais zaidi ya kikomo cha mihula miwili inayotumika sasa.

Mswada wa kura ya maoni uliopitishwa kwa mara ya kwanza mwezi Juni na kuidhinishwa na mahakama ya Katiba mwezi Agosti, umetajwa kuwa chanzo kikuu cha maandamano hayo.

Uchaguzi Mkuu nchni DRC, utaandaliwa katika muda wa miaka miwili ijayo, lakini hali ya taharuki inazidi kutanda kati ya serikali na upinzani, baada ya bunge kupendekeza kuongezwa kwa muhula wa Rais.

Share This Article