Chama United Democratic Alliance UDA, leo Jumamosi kinaandaa marudio ya awamu ya tatu ya uchaguzi wa mashinani katika kaunti 18.
Kaunti hizo ni pamoja na Samburu, Trans Nzoia, Vihiga, Elgeyo Marakwet, Baringo, Uasin Gishu, Nandi, Kericho, Bomet, Nyandarua na Laikipia.
Zingne ni kaunti ya Meru, Tharaka Nithi, Embu, Kirinyaga, Nyeri, Murang’a na Kiambu.
Mwenyekiti wa chama cha UDA ambaye ni Gavana wa Embu Cecily Mbarire, amesema uchaguzi huo utafanyika kwa njia ya kidijitali ili kudumishaa uwazi.
Aliwataka wanachama waliosajiliwa wa chama hicho kujiokeza kwa wingi kuwachagua wawakilishi wao wa viwango vyote vya uongozi wa chama hicho.
Uchaguzi huo awali uliahirishwa kufuatia kifo cha mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng’eno, ambaye alikuwa mwanachama wa bodi ya uchaguzi ya chama hicho.