Ubalozi wa Ureno jijini Nairobi ulianza kujitegemea kutengeneza VIZA kwa Wakenya wanaonuia kuzuru nchini Ureno.
Ubalozi huo ulianza kutoa stakabadhi hiyo muhimu tarehe tano mwezi huu, baada ya kujiondoa kwa wakala ambaye amekuwa akiandaa Viza kwa niaba ya Ureno pamoja na mataifa yote ya eneo la Schengen
Yamkimi mkataba huo wa wakala wa Ugiriki ulikamilika tarehe mosi mwezi huu.
Wakenya wanaotaka Viza za Ureno ni sharti wafike katika ubalozi wa Ureno humu nchini.