Tuzo za 22 za SOYA kuandaliwa Ijumaa usiku

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya 22 ya tuzo za wanamichezo bora wa mwaka 2025 za SOYA zitaandaliwa Ijumaa usiku eneo la Uhuru Gardens kaunti ya Nairobi.

Mabingwa wa Dunia Beatrice Chebet na Emmanuel Wanyonyi wanawania kuhifadhi tuzo za mwaka jana  za mwanamke bora na mwanaume bora mtawalia.

Wanamichezo watatuzwa katika vitengo 16 tofauti katika hafla itakayohudhuriwa na mshikilizi wa zamani wa rekodi ya Dunia katika marathon Haile Gebrselassie wa Ethiopia.

Chebet  anawania tuzo ya mwanamke bora Pamoja na mabingwa wenza wa dunia akina Faith Kipyegon,Faith Cherotich,Lillian Odira na mchezaji kitara mzawa wa Ujerumani Alexandra Ndolo.

Wanyonyi  anawania tuzo ya wanaume Pamoja na mshambulizi wa Harambee Stars Ryan Ogam, mcheza gofu Njoroge Kibugu, mshambulizi wa Nairobi City Thunder Albert Odero, na bingwa wa  Berlin marathon Sabastian Sawe.

TAGGED:
Share This Article