Rais William Ruto Jumatatu jioni alikutana na Rais wa Shirika la kimataifa la kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini michezoni (WADA) Ban̈ka Witold.
Ruto alikariri kuwa Kenya inashirikiana kwa karibu na WADA kuhakikisha wanariadha wanashindana kwa haki bila matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Aliongeza kuwa Kenya imepiga hatua kubwa tangu ilipobuni sheria ya kukabiliana na dawa haramu michezoni mwaka 2016.
Aidha,Ruto alisema Kenya inawianisha sheria za sasa na zile za WADA huku sheria hiyo mpya ikitarajiwa kuanza kutekelezwa Januari mwaka ujao.

Miomngoni mwa sheria zinazotarajiwa kutekelezwa nchini Kenya kuanzia mwaka ujao ni kufanya makosa ya ulaji muku kuwa makosa ya uhalifu.
Witold anayezuru nchini Kenya kwa mara ya kwanza na aliye kwenye ziara rasmi ya siku tatu atakutana na mashirikisho ya michezo na wanamichezo siku ya Jumanne hali kadhalika kamati ya Olimpiki NOC-K kabla ya kuwahutubia Wanahabari.