Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa Marekani inaendelea kufanya mazungumzo na Iran, lakini amesisitiza kuwa usitishaji wa mapigano umefikia mwisho.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Trump alisema: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuomba kuendelea na mazungumzo. Tumekubali ombi hilo, lakini Marekani imewaeleza wazi kwamba usitishaji wa mapigano umekwisha.”
Kauli hiyo imekuja baada ya Marekani kushambulia maeneo kadhaa katika majimbo matano kusini mwa Iran, kufuatia mashambulizi dhidi ya meli zilizokuwa zikipita eneo hilo, Washington ikiilaumu Iran kwa mashambulizi hayo.
Aidha, maafisa wa Iran wamesema nchi hiyo ina haki ya kujibu mashambulizi yoyote yanayolenga miundombinu yake.
Taarifa ya BBC