Starlets wailambisha India pilipili na kufuzu kumenyana na Australia fainalini

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya kwa wanawake ,Harambee Starlets itachuana na miamba Australia, katika fainali ya mechi za kirafiki za FIFA series wiki ijayo.

Hii ni baada ya kuibwaga India Jumamosi katika nusu fainali ya pili iliyotitigwa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo,Martha Amunyolete, akitikisa wavu wa India kunako dakika ya pili kabla ya Tereza Engesha kutanua uongozi kwa goli la pili dakika ya 57.

Awali Australia walitinga fainali baada ya kuwagaragaza Malawi magoli 5 bila jawabu katika nusu fainali ya kwanza.

Starlets watashuka uwanjani Aprili 15 kwa fainali ambayo itatanguliwa na mchuano wa kuwania nafasi ya tatu na nne kati ya India na Malawi.

Share This Article