Sonko achaguliwa Mlezi wa Bodaboda na Tuktuk

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko, amechaguliwa kuwa mlezi wa chama wamiliki wa Bodaboda na Tuktuk humu nchini.

Sonko amechaguliwa Jumapili na viongozi wa vyama vya wamiliki wa bodaboda na Tuktuk, wanaowakilisha wanachama zaidi ya milioni 2.5.

Kwenye mkutano ulioandaliwa leo katika shamba la Sonko Mua Farm, kaunti ya Machakos, viongozi hao walielezea matumaini yao na uwakilishi wa Sonko katika wadhfa huo na kuwasilisha ajenda yao ipasavyo.

Sonko amekubali uteuzi huo na kuahidi kutetea haki za wanabodaboda na wamiliki wa Tuktuk nchini, akisema atashirikisha serikali za kaunti na ile ya kitaifa kuhakisha haki zao hazikiukwi.

Aidha, Gavana huyo wa zamani amesema atakutana na Seneta Bonny Khalwale kujadili changamoto zinazokumba sekta hiyo nchini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *