Solberg ashikilia kukutu uongozi wa Safari Rally

Dismas Otuke
1 Min Read
Oliver Solberg akiwa mashindanoni. Picha hisani ya SM

Dereva wa kutoka Uswidi Oliver Solberg anaongoza mashindano ya mbio za magari ya WRC Safari Rally baada ya kukamilika kwa vituo sita vya mashindano Ijumaa adhuhuri mjini Naivasha.

Solberg wa kampuni ya magari ya Toyota anaongoza kwa kuwa na muda wa kasi wa dakika 58 sekunde 30.3, akifuatwa na wenzake wa Toyota katika nafasi nne za kwanza, Elfyn Evans, Sebastien Ogier na Takamoto Katsuta, walioshikilia nafasi za pili, tatu na nne mtawalia.

Karan Patel, akiendesha gari aina ya Skoda Fabia akishiriki kitengo cha pili cha WRC, ndiye dereva bora wa Kenya katika nafasi ya 16, akifuatwa na Aakif Virani aliye wa 18.

Awali, Ijumaa, kituo cha kwanza cha mashindano cha Camp Moran 2 kilifutiliwa mbali kutokana na matope mengi kwenye barabara hiyo.

Share This Article