Ndoto ya klabu ya Simba kutoka Tanzania bara, kutwaa kombe la shirikisho ilitibuka Jumapili jioni baada ya RS Berkane kunyakua kombe hilo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.
Simba walitoka sare ya bao 1 katika marudio ya fainali uwanjani Amaan kisiwani Zanzibar .
Berkane walikuwa wamesajili ushindi wa mabao 2-0, katika duru ya kwanza wiki jana wakiwa nyumbani.
Berkane wametuzwa dola milioni 2, huku Simba wakipokea dola milioni moja za Marekani kwa kumaliza nafasi ya pili.