Shabana yailewesha Tusker, Ingwe watesa matarishi Posta

Dismas Otuke
1 Min Read

Shabana FC ilizidisha masaibu ya mabingwa wa zamani Tukser FC walipowanyuka bao moja bila jawabu katika mechi ya Ligi Kuu ya Sportpesa iliyopigwa Jumamosi katika uwanja wa Gus. ii.

AFC Leopards walisajili ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Posta Rangers ugani Nyayo, nao Bandari FC wakainyuka Murang’a Seal magoli 3-2 katika kiwara cha Sportpesa.

Kwenye matokeo mengine, Mathare United walilazimishwa kutoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Kariobangi Sharks uwanjani Police Sacco.

Share This Article