Serikali yaweka mikakati kuzuia ongezeko la bei za bidhaa muhimu nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amesema serikali imeweka mikakati ifaayo ya kuzuia ongezeko la bidhaa muhimu za matumizi zinazoagizwa humu nchini kutokana na mtafaruku unaoendelea eneo la ghuba.

Kwenya taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni, Rais amesema amepokea ripoti kutoka kwa Wizara za Nishati, Biashara, Fedha, Kilimo pamoja na Benki Kuu na wadau wa sekta za kibinafsi iliyotoa mapendekezo ya kudhibiti bei ya bidhaa muhimu.

Rais ametoa hakikisho la kuwepo kwa akiba toshelezi ya mafuta ambayo itazuia upungufu wowote ambao ungepandisha bei yake kutokana na mpango uliowekwa wa kununua mafuta moja kwa moja kutoka wazalishaji mafuta huko Mashariki ya Kati.

Kuhusu mbolea, Ruto ametoa hakikisho kwa wakulima kuwa hakutakuwa na changamoto yoyote wala upungufu wake humu nchini wakati huu wa msimu wa upanzi.

Hata hivyo, Rais amekiri kuwepo kwa changamoto katika sekta ya uagizaji na uuzaji nyama nje ya nchi kutokana na matatizo ya usafiri wa kimataifa.

Share This Article