Serikali yatoa shilingi bilioni 3.2 za mpango wa Inua Jamii

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya Leba na ulinzi wa jamii imetoa shilingi bilioni 3.2 yakiwia  malipo ya mwezi Juni  chini ya mpango wa  Inua Jamii.

Malipo hayo yanalenga kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum katika jamii wakiwemo yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu, wazee, watu wenye ulemavu  na wale walio chini ya mpango wa kupokea msaada wa vyakula.

Katibu  wa ulinzi wa jamii Joseph Motari, amesema wamesajili watu 570,263 wapya wamesajiliwa  katika mpango wa Inua Jamii  na kufikisha idadi ya watu 1,607,996 kufikiwa mwisho wa mwezi Juni mwaka huu.

Motari ameongeza kuwa walionufaika watapokea  malipo kuanzia  Jumatano hii kupitia kwa akaunti za benki.

Mpango huo ulipanuliwa kufuatia agizo la Rais William Ruto  mwaka jana aliyetaka idadi ya wanaonufaika kuongezwa hadi   kufikia watu milioni 2.5.

Mpango wa Inua Jamii ni mpango wa serikali uliobuniwa  ili kutoa msaada wa kifedha kwa makundi mbalimbali ya jamii, kuwasaidia kukidhi mahitaji yao ya kimsingi na kuboresha maisha yao .

 

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *