Waziri wa Elimu Julius Ogamba inahitaji shilingi bilioni 23 zaidi ili kuwaajiri wa limu wa Junior Secondary kwa kandarasi za kudumu .
Ogamba amesema kulinga na agizo la mahakama na kusema ilikuwa kinyume cha sheria kuwaajiri walimu hao kwa kandarasi fupi,ni vigumu kuwapa walimu kandarasi za kudumu kutokana na uhaba wa pesa.
Waziri Ogamba amesema kwa sasa serikali ina shilingi bilioni 6 pekee kwa zoezi hilo.
Amesisitiza kuwa walimu hao wataajiriwa kwa awamu kulingana na uwepo wa fedha.
Jumla ya walimu 20,000 wanapaswa kupewa kandarasi za muda mrefu.