Ruto: Serikali iliimarisha Linda Mama, haikuifutilia mbali

Ruto alifafanua kuwa mpango wa Linda Jamii unawasaidia kina mama wanapokuwa wajawazito, wanapojifungua na hata baada ya kujifungua.

Tom Mathinji
2 Min Read
William Ruto - Rais wa Kenya
Rais  William Ruto, amepuuzilia mbali madai kwamba utawala wake uliondolea mbali mpango wa Linda Mama, akidokeza kuwa mpango huo uliimarishwa na kuwa Linda Jamii.
Kulingana na Rais mpango wa Linda Jamii unatoa huduma pana za afya, zilizo na manufaa mengi kwa kina mama wajawazito, watoto wachanga na familia zilizo chini ya Halmashauri ya Afya ya Jamii  (SHA).

Akizungumza leo Alhamisi katika Ikulu ya Nairobi  kwenye mkutano na mafundi mbalimbali wa kaunti ya Nairobi, kiongozi wa taifa alifafanua kuwa mpango wa Linda Jamii unawasaidia kina mama wanapokuwa wajawazito, wanapojifungua na hata baada ya kujifungua.

“Tulikuwa na mpango wa Linda Mama, sasa ni Linda Jamii. Kila mama, Serikali ya Kenya itakulipia kwenda clinic hadi wakati  na baada ya kujifungua,” President Ruto said.

Alisema serikali imeongeza ufadhili wa huduma za kina mama wajawazito, ili kuimarisha ubora na kupunguza vifo vinavyotokana na ujauzito na  maafa ya watoto wanaozaliwa.

“Zamani, bajeti ya mama kujifungua hospitalini ilikuwa shilingi 4,000. Kwa sasa kupitia mpango wa Linda Jamii bajeti hiyo tumeongeza mara tatu kuhakikisha kwamba kila mama anajifungua mahali ambapo kuna usafi, kuna daktari, dawa na tusipoteze wamama ama watoto wakati wa kujifungua,” he said.

Rais alishikilia kuwa mabadiliko hayo ni sehemu ya mpango mpana wa kutimiza utoaji huduma za afya kwa wote kupitia Halmashauri ya Afya ya Jamii, kuhakikisha kila Mkenya anapata huduma za afya bila kujali hali zao za kifedha.

Share This Article