Shirikisho la Riadha Duniani limerasmisha rekodi ya Dunia ya Marathon yake Mkenya Sabastian Sawe ya mwezi Aprili mwaka huu katika mbio za London Marathon.
Sawe alitwaa ubingwa wa mbio hizo kwa muda wa saa 1, dakika 59 na sekunde 30 na hivyo kuwa mwanamume wa kwanza kukamilisha mbio za marathoni za kilomita 42 chini ya saa mbili.
Mwanariadha huyo kutoka kaunti ya Nandi, aliboresha rekodi ya awali kwa sekunde 65 ya Mkenya mwenza marehemu Kelvin Kiptum, iliyoandikishwa katika mbio za Chicago Marathon Oktoba 8 mwaka 2023.