Rais Felix Tshisekedi ametuza kila mchezaji wa timu ya taifa ya soka shilingi milioni 130, baada ya kuandikisha historia ilipofuzu kwa Kombe la dunia mwaka huu kwa mara ya kwanza baada ya subira ya miaka 52 walipoishinda Jamaica bao moja kwa bila.
Aidha, kila mchezaji wa kikosi hicho atapewa ploti na gari jipya aina ya Jeep na kupokea Pasipoti ya watu maarufu.
DRC itakuwa timu ya 10 ya Afrika kushiriki Kombe la Dunia mwaka huu.
Chui wa Congo wamo kundi K la Kombe la Dunia mwaka huu katika mataifa ya Marekani,Canada na Mexico pamoja na Ureno,Uzibekistan na Colombia.