Rais Ruto:Ushirikiano wa Kenya na Marekani ni wa kirafiki 

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ametaja ushirikiano baina ya Kenya na Marekani kuwa wa kirafiki unaogemea maslahi ya mataifa hayo mawili.

Rais alisema haya jana jioni alipokutana na viongozi wa bunge la Congress kutoka nchini Marekani, waliomtembelea katika Ikulu ya Nairobi.

Aidha, Ruto na viongozi hao walijadiliana kwa kina kuhusu mchango wa shirika la ukuaji wa bara Afrika na upatikanaji wa fursa (AGOA), ambalo bidhaa nyingi za humu nchini hupitia kabla ya kuingia katika soko la Marekani.

Kenya na Marekani hushirikiana katika sekta za  biashara,Afya,usalama wa kikanda,usalama na ulinzi.

Viongozi hao walikuwa Lola Zinke, Tom Suozzi, Guy Reschenthaler, na Julia Brownley.

Share This Article