Rais William Ruto leo Alhamisi yuko kwenye ziara katika kaunti ya Nandi.
Wakati wa ziara hiyo, Ruto anatarajiwa kukagua miradi kadhaa ya maendeleo na kufungua nyingine pamoja na kuwahutubia wananchi.
Ruto ameanzisha ujenzi wa mabweni ya shule ya upili ya wasichana ya St. Joseph’s Chepterit na kutoa basi la shule.
Aidha, Rais ameahidi kujenga ukumbi unaotoshea idadi ya wanafunzi 2,500, ofisi na madarasa 30 zaidi pamoja na kutoa tarakilishi 100 kwa shule hiyo ifikapo mwezi Mei mwaka huu.
Kiongozi wa nchi ameongeza kuwa lengo lake ni kuongeza idadi ya wanafunzi shuleni humo hadi 3,200 kutoka idadi ya sasa ya wanafunzi 1,600.