Rais Ruto azindua huduma ya usafiri wa reli ya Mombasa

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amezindua huduma za uchukuzi wa reli ya Mombasa kutoka kituo cha  Mariakani hadi jijini Mombasa.

Reli hiyo ya umbali wa kilomita 16.6 la kisasa linajumuisha daraja linalopita juu ya Bahari Hindi la umbali wa kilomita 2.3 katika eneo la Makupa.

Gari moshi hilo litaunganisha reli ya kisasa ya SGR kutoka Miritini hadi kuingia katikati ya mji wa Mombasa.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir pamoja na Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir.

Share This Article