Rais William Ruto mapema Alhamisi amekabidhi hati za kuanza kutoa mafunzo kwa vyuo vikuu vya Kenya Advanced Institute of Science and Technology (KAIST) na Kenya Medical Research Institute (KEMRI), katika hafla iliyoandaliwa katika Ikulu ya Nairobi.
Akizungumza baada ya kutoa hati hizo Rais, alisema hatua hiyo inalenga kupanua fursa za utoaji mafunzo ya vyuo vikuu nchini na kuimarisha uvumbuzi,Sayansi pamoja na utafiti.

“Vyuo vikuu vinatakeleza wajibu muhimu katika kutoa mafunzo kwa Wanasayansi,Wahandisi,Madaktari na Wavumbuzi, watakaoongeza maarifa na kubadilisha mtazamo wa taifa na Ulimwenguni.”akasema Rais Ruto
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mawaziri Aden Duale wa Afya,William Kabogo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Julius Ogamba wa Elimu.