Rais William Ruto jana Jumatano jioni alikutana na baadhi viongozi kutoka kaunti ya Machakos ambapo walijadiliana jinsi ya kuinua eneo hilo kimaendeleo.
Alikariri nia yake ya kulikwamua eneo hilo kimaendeleo baada ya kusalia nyuma kwa muda mrefu zaidi.
Ruto aliongeza kuwa serikali yake kamwe haitakubali kaunti ya Machakos kukosa kunufaika kupata miradi ya maendeleo.
Wabunge waliomtembelea Rais Ikuluni ni pamoja na wabunge Vincent Kawaya wa Mwala, Fabian Muli wa Kangundo, Joshua Mwalyo wa Masinga na aliyekuwa msimamiziwa Ikulu Nzioka Waita.
Nzioka aligombea ugaavana wa kaunti ya Machakos katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 lakini akabwagwa na Gavana wa sasa Wavinya Ndeti.
Haijabainika ikiwa atajaribu tena bahati yake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Mbunge wa Mavoko Patrick Makau tayari ameelezea nia ya kumbandua Ndeti kwenye wadhifa huo katika uchaguzi huo.