Raia wa Palestina wanashiriki upigaji kura za manispaa katika eneo la Gaza ya kati na Magharibi mwa ukingo wa mto Jordan, hizi zikiwa chaguzi za kwanza tangu mwaka 2006.
Vituo vya kupiga kura vilifunguliwa saa moja asubuhi saa za nchini humo, huku wapiga kura 70,000 waliosajiliwa wakishiriki zoezi hilo katika eneo la Deir al-Balah katikati mwa Gaza ambako kundi la Hamas linaendesha shughuli zake.
Kundi la Hamas halikuruhusiwa kuwa na wagombeaji kwenye uchaguzi huo na makundi megine kadhaa yaliususia kwasababu ya hitaji la kuwataka wagombeaji watambue utawala wa chama cha Palestinian Liberation Organisation (PLO), ambacho kina uwezo mkubwa katika serikali ya Palestina inayotawala sehemu za ukingo wa magharibi ya mto Jodan zisikuwa chini ya utawala wa Israeli.
FATAH,kundi linaloongozwa na Rais Mahmoud Abbas na lililo na ushawishi mkubwa katika chama cha PLO, liliondolewa Gaza na Hamas baada ya uchaguzi uliopita.
Zaidi ya wapiga kura millioni moja katika maeneo ya wapalestina wamesajiliwa kuwa wapiga kura,wakiwemo wapiga kura elfu 70 katika eneo la Deir al-Balah,lililo nan a vituo 12 vya kupigia kura.