Mwanamke raia wa Canada ameuawa, huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya mwanaume aliyekuwa amejihami kufyatua risasi kiholela katika kituo cha kitalii huko Mexico, hayo ni kulingana na maafisa wa serikali wa Mexico.
Tukio hilo lilijiri katika eneo la utafiti wa alikotoka mwanadamu la Teotihuacán kaskazini mwa jiji la Mexico. Mwanaume huyo baadaye alijitoa uai kwa kujipiga risasi.
Polisi walipata bunduki aliyotumia na maganda ya risasi. Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum alisema anafuatilia matukio kuhusiana na tukio hilo na kwamba anashauriana na ubalozi wa Canada nchini humo.
Kituo hicho cha kitalii cha Teotihuacán cha Unesco ni mojawpao wa maeneo yanayowavutia watalii wengi nchini humo. Sheinbaum amesema ameagiza waziri wake wa usalama kuchunguza kisa hicho na kutoa msaada ufaao.
Waziri wa usalama Cristóbal Castañeda Camarillo, aliambia waandishi wa habari kwamba raia wawili wa Colombia, mmoja wa Urusi na mwingine wa Canada ni miongoni mwa amajeruhi.