Paul Biya amteua mwanawe kuwa Makamu wa Rais wa kwanza nchini Cameroon

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Cameroon Paul Biya amemteua mwanawe Franck Emmanuel Biya kuwa Makamu wa kwanza wa Rais katika hatua ambayo imeibua mjadala mkubwa nchini humo.

Uteuzi huo ulitangazwa Aprili 4 huku pia mwanawe akihudumu  katika wadhfa wa Mkuu wa Majeshi na anashikilia wadhifa mkubwa katika Wizara ya Ulinzi kama njia ya kudhibiti nchi.

Haya yalijiri siku chache baada ya bunge la taifa hilo kupiga kura kurejesha wadhifa wa Makamu Rais kama njia ya kuhakikisha hakuna pengo la uongozi hususan Rais Biya akiwa na umri wa miaka 93.

Biya amekuwa mamlakani tangu mwaka 1982 na alishinda muhula wa nane afisini kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita.

Kikao cha pamoja cha mabunge mawili nchini Cameroon kilipitisha mswada wa kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo ya Afrika ya Kati Jumamosi iliyopita.

Wabunge 200 waliunga mkono kubuniwa kwa nafasi ya Naibu Rais huku 18 pekee wakipinga.

Share This Article