Ni mguu niponye polisi wakitumia vitoza machozi Kikuyu

Dismas Otuke
1 Min Read

Maelfu ya wafuasi waliofika kuhudhuria mikutano ya kisiasa iliyoongozwa na viongozi wa upinzani wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Rais  Rigathi Gachagua,katika mji wa Kikuyu walijipata wakiparakasa masafa baada ya maafisa wa polisi kulazimika kutumia vitoza machozi ili kuwatawanya.

Yamkini vurugumechi zilianza wakati wa makabiliano baina ya wafuasi wa viongozi wa upinzani dhidi ya kundi jingine lililojaribu kufunga barabara  ya Southern Bypass za kuingia Kikuyu kwa kutumia mawe na kuchoma magurudumu.

Polisi walifanikiwa kutuliza hali licha ya makabiliano makali.

Upinzani umeishutumu serikali kwa kutumia nguvu kupita kiasi huku mbunge wa eneo hilo ambaye pia ni kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichuingwah,akiahidi kuwa serikali itawachukulia hatua kali viongozi wa upinzani waliohusika katika vurumai hizo na uharibifu wa mali.

TAGGED:
Share This Article