Nepal yaonya kuhusu mafuriko zaidi, watu 3,000 hawajulikani walipo

Vifo vilivyotokana na mafuriko ynchini Nepal, na eneo la Tibet nchini China vimepanda na kufikia 800 huku zaidi ya watu 3,000 wakiwa hawajulikani waliko.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Nepal imeonya kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa mafuriko zaidi, ikiwataka wakazi walio karibu na maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ya wiki jana kuhama huku viwango vya maji katika mto wa Bhotekoshi vikipanda.

Serikali ilituma jumbe kwa rununu za raia wake mapema jana Jumapili  kuwatahadharisha juu ya kutokea kwa mafuriko zaidi katika maeneo mengine ikiwemo barabara kuu ya Kathmandu, iliyoathiriwa katika mafuriko ya wiki jana.

Vifo vilivyotokana na mafuriko ynchini Nepal, na eneo la Tibet nchini China vimepanda na kufikia 800 huku zaidi ya watu 3,000 wakiwa hawajulikani waliko.

Nepal imetangaza jumla ya vifo 734 huku watu 498 wakiwa hawajulikani waliko, ilhali serikali ya China imeripoti vifo 16 na watu wengine 546 hawajulikani walipo.

Watu wapatao 93,000 nchini Nepal wameathiriwa na mkasa huo mbaya zaidi kuwahi kutokea kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Share This Article