Wakazi wa Jiji la Nairobi, walitatizika na shughuli za uchukuzi kutokana na mvua mkubwa ambayo ilishuhudiwa.
Mvua hiyo ilisababisha mafuriko makubwa barabarani, na kukwamiaha usafiri wa magari na wanaotembea kwa miguu.
Uchunguzi uliofanywa na Shirika la Utangazaji KBC, watu wengi walikwama barabarani baada ya kukosa huduma za uchukuzi
Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini imesema mvua hiyo itaendelea Jijini Nairobi hadi tarehe tisa mwezi huu.
Utabiri huo unaonyesha mvua hiyo itakithiri katika kipindi cha saa 24 zijazo hapa Nairobi.
Kaunti jirani za Kiambu , Machakos na baadhi ya maeneo ya kaunti ya Kajiado pia zinatarajiwa kupokea mvua kubwa.
Maafisa wameonya kuwa mvua hiyo huenda ikasababisha mafuriko pamoja na kukatiza shughuli za uchukuzi wa barabara.
Wakazi wameshauriwa kuepuka barabara zilizofurika wakati wa mvua.