Museveni aombwa kuelekeza pesa za wabunifu kwa mafuriko

Rais Museveni alikutana na waunda maudhui mitandaoni akaahidi kutoa shilingi bilioni 5 kupiga jeki chama chao cha akiba na mikopo.

Marion Bosire
1 Min Read
Biswanka, Mwanamuziki wa Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameombwa aelekeze shilingi bilioni 5 za Uganda alizoahidi wabunifu kwa kushughulikia athari za mafuriko jijini Kampala.

Mwanamuziki wa Uganda Derrick Biswanka alitoa ombi hilo kwa Rais Museveni kupitia akaunti yake ya mtandao wa Facebook.

Ikumbukwe kwamba wiki chache zilizopita, Rais Museveni katika makazi yake ya Kisozi, alikutana na waunda maudhui mitandaoni ambapo aliahidi kutoa shilingi bilioni 5 kupiga jeki chama chao cha akiba na mikopo.

Rais aliahidi kuwasilisha mchango huo kupitia kwa mmoja wa wanamitandao hao maarufu kama Kasuku na sasa Biswanka anamtaka Rais atoe pesa hizo kama fidia kwa aliopoteza mali na maisha katika mafuriko jijini Kampala.

Huku hayo yakijiri, mchango huo alioahidi Museveni umekuwa ikikejeliwa na wengi wanaoshangaa jinsi pesa hizo zitatumiwa na ni kwa nini mchang huo umetolwewa wakati ambapo kuna masuala muhimu na ya dharura.

Share This Article