Mudavadi: Kenya inadhamini ushirikiano wake na Ireland

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, amesema kuwa Kenya inadhamini zaidi ushirikiano wake na taifa la Ireland.

Alisema mashirika ya Ireland yanayohudumu hapa nchini, yamefanikisha ukuaji wa kiuchumi na kijamii pamoja na ushirikiano baina ya raia wa nchi hizo mbili.

Mudavadi alidokeza kuwa Kenya inajizatiti kuimarisha ushirikiano huo hasaa katika sekta za biashara, maendeleo na fursa zingine za kimataifa.

Aliyasema hayo  siku ya Ijumaa alipohudhuria siku ya kimataifa ya Ireland, iliyoandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Christopher O’Sullivan na balozi wa nchi hiyo hapa Kenya Caitríona Ingoldsby.

Kwenye hafla hiyo, Mudavadi aliwasilisha rambirambi za Kenya kwa taifa la Ireland, huku akihakikisha kuendeleza ushirikiano na taifa hilo.

Share This Article