Mmoja afariki, 4 waokolewa baada ya jengo kuanguka Kericho

Tom Mathinji
1 Min Read
Jengo lililokuwa likijengwa laporomoka Kericho.

Mtu mmoja amefariki baada ya jengo lililokuwa likijengwa kuporomoka katika eneo la Chebocho kaunti ya Kericho.

Akithibitisha mkasa huo, Kamishna wa kaunti ya Kericho Jeremiah Gicheru, amesema mwili huo umeondolewa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Kericho.

Kulingana na Gicheru, watu wanne wameokolewa na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya kaunti ya kericho kwa matibabu, huku shughuli zikiendelea za kubaini ni watu wanganpi waliwemo jengo hilo lilipoanguka.

Kwenye taarifa Jumatano usiku, Gicheru alisema vikosi vya uokoaji kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu na Maafisa wa Serikali ya Kitaifa, tayari vimepelekwa kwenye eneo hilo.

“Shughuli za uokoaji tayari zinaendelea, Hadi sasa watu wanne wameokolewa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya kericho kwa matibabu,” alisema Gicheru.

Share This Article