Maafisa wa polisi kaunti ya Kakamega wamemkamata mshukiwa wa ujambazi Jackson Mwangi Wangechi, mwenye umri wa miaka 38, ambaye alipataka na silaha baada ya polisi kutekeleza operesheni katika maficho yake matatu.
Baada ya kupokea habari za kijasusi, maafisa hao wa polisi walimfumania mshukiwa huyo katika eneo noja la burudani katika mji wa Malava, kabla ya kuandamana naye hadi nyumbani kwake ambapo silaha hizo zilipatikana.
Silaha zilizopatikana zilijumuisha vifaa vya kuvunja, mavazi ya kijeshi, risasi za mipira, bastola mbili, shoka, rununu zinazoshukiwa kuwa za wizi, vifunguo na vifaa vya mawasiliano.
Kupitia mtandao wa X, idara ya upelelezi wa makosa ya jinai ilisema maafisa hao waliandamana na mshukiwa huyo hadi katika maficho mengine mawili ambapo walipata panga, funguo zilzopatikana ndani ya gari aina ya Mazda Demio yenye nambari za usajili KDL 013B.
Kwa sasa mshukiwa huyo anazuiliwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea.