Msamaha kuhusu makala ya Naibu Rais wa Cameroon

Tom Mathinji
1 Min Read

Mnamo siku ya Jumatatu Aprili 6, 2026, KBC Digital ilichapisha habari kuwa Rais wa Cameroon Paul Biya amemteua mwanawe wa kiume,  Franck Emmanuel Biya, kuwa Makamu wa Rais wa taifa hilo.

Hata hivyo, imebainika kuwa bahari hizo hazikuwa sahihi na kwamba hakuna uteuzi rasmi kwenye wadhifa huo ulifanywa.  KBC Digital imeondoa taarifa hiyo na inachukua fursa hii kuomba msamaha wa dhati kutokana na hofu iliyosababishwa na taarifa hiyo. Tunakariri azma yetu ya daima kuchapisha taarifa sahihi.

TAGGED:
Share This Article