Msaidizi wangu alinishambulia wakati akiomba, asema rubani wa Flydubai

Smit Machchhar kutoka India amefichua kuwa alishambuliwa kutokea nyuma baada ya kumruhusu msaidizi wake kuomba kwa dakika chache.

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya NDTV

Rubani wa ndege ya abiria ya Flydubai Smit Machchhar ameendelea kuelezea kilichotokea angani wiki jana kabla ya ndege hiyo kunusurika kuanguka.

Machchhar kutoka India amefichua kuwa alishambuliwa kutokea nyuma baada ya kumruhusu msaidizi wake kuomba kwa dakika chache.

Aliyasema hayo wakati wa mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu juzi Jumamosi.

Rubani wake msaidizi, anayeripotiwa kutokea Oman, alimshambulia Alhamisi wiki iliyopita wakati wa safari ya ndege kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE kuelekea nchini Israel.

Machchhar alisema msaidizi wake alimwarifu kuwa alitaka kuomba, na rubani huyo hakugeuka kumtazama wakati kipindi hicho cha maombi. Takriban dakika tano baadaye, alishambuliwa ghafla kutoka nyuma.

Rubani huyo alisema alijaribu kumzuia mshambuliaji lakini uwezo wake wa kuona ulififia kutokana na mapigo ya awali.

Ripoti zinaashiria rubani msaidizi alijaribu kuiangusha ndege hiyo baada ya kumshambulia Machchhar.

Sababu za kumshambulia mwenzake bado hazijulikani.

Share This Article