Mlinzi wa Raila wa muda mrefu George Oduor afariki

Dismas Otuke
1 Min Read

Mlinzi wa Raila Odinga wa muda mrefu George Oduor ameaga dunia. 

Oduor alifariki jana Jumatano jioni katika hospitali moja jijini Nairobi, alikokuwa anapokea matibabu.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Raila, Oduor alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kupitia kwa mitandao ya kijamii, kinara huyo wa chama cha ODM alimtaja Oduor kuwa rafiki wa karibu wa familia yao tangu mwisho mwisho wa miaka ya 1980.

Aidha, alimsifia Oduor kuwa mtulivu, aliyemakinika kazini na mtaalam wa kazi  yake na aliyesimama tisti naye katika nyakati ngumu.

Raila pia ametoa risala za rambirambi kwa mjane Carol, ndugu, jamaa na marafiki.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *