Baraza la mitihani nchini Tanzania (Necta) limerudisha mbele tarehe ya kuanza kwa mitihani ya kitaifa kutokana na mvua ya El Nino inayotarajiwa kuanzia mwishoni mwa Oktoba katika maeneo mengini nchini humo.
Kulinagna na Naibu waziri wa Elimu Wanu Hafidh ,mitahani hiyo iliyokuwa iandaliwa kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu ili kuhakikisha usalama wa mitihani,wanafunzi na wasimamizi.
Katibu mtendaji wa Necta Professa Said Mohamed amesema mtihaji wa utathmini kwa wanafunzi wa darasa la nne utaandaliwa kati ya Oktoba 5 na 6 badala ya Oktoba 21 na 22.
Mtihani wa utathmini wa kitaifa wa darasa la pili ulioratibiwa kuandalia Novemba 17 na 18 sasa utaandaliwa Oktoba 7 na 8.
Aidha,mtihani wa kitaifa wa kidato cha pili uliokuwa ufanywe baina ya Novemba 2 na 13 sasa utaandaliwa kati ya Oktoba 12 na 23, huku mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne uliokuwa uandaliwe baina ya Novemba 9 na 27, sasa utafanyika kuanzia Oktoba 19 hadi Novemba 6.