Miili 23 ya watu waliosombwa na maji yaopolewa Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read

Huduma ya kitaifa ya polisi imetangaza kuwa imepata miili 23 ya watu waliosombwa na mafuriko ya maji kufuatia mvua kubwa iliyoshudiwa katika kaunti ya Nairobi Ijumaa usiku.

Mvua hiyo ilisababisha mafuriko yaliyofunga barabara nyingi jijini na kukatiza usafiri huku magari, watu na mali zikisombwa na maji.

Kwa mujibu wa polisi, mitaa iliyoathiriwa na mafuriko ya Ijumaa usiku ni pamoja na Mukuru, Kibra, Mathare, Huruma, South B, Embakasi, Roysambu, Kahawa West na maeneo mengi ya Westlands.

Aidha, polisi walifanikiwa kuwanusuru watu wengine 29 waliokuwa wamekwama kwenye mafuriko hayo.

Polisi imewataka Wakenya kupiga nambari za simu za dharura ili kupata msaada wakati wa mafuriko zikiwa 999, 112 na 911.

Share This Article