Mechi za marudiano za awamu ya timu 16 kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya (UEFA) zitachezwa leo Jumanne usiku.
Kwenye mechi hizo, timu ya Manchester City itachuana na Real Madrid katika uwanja wa Etihad, huku ikilenga kushinda mechi hiyo ili ijipatie matumaini ya kufuzu kwa robo fainali.
Kwenye mkutano na wanahabari, kocha wa Manchester City Pep Guardiola aliweka wazi kuwa ana imani na kikosi chake, na watajituma vilivyo kuzoa ushindi na kufuzu kwa hatua ya robo fainali.
Wakati huo huo, Real Madrid itakuwa inalenga kutoka sare ama kushinda mechi hiyo ili kufuzu kwa robo fainali.
Katika mechi zingine, Chelsea itachuana na PSG, Arsenal imenyane na Bayer Levakusen nayo Sporting CP itoane jasho na Bodoe Glimt.