Marekani yafunga ubalozi Nairobi kuadhimisha sikukuu

Huduma za kawaida katika ubalozi huo zinatarajiwa kurejea kesho, Ijumaa, Novemba 27, 2026.

Marion Bosire
1 Min Read

Serikali ya Marekani imefunga kwa muda ubalozi wake jijini Nairobi leo, Alhamisi, Novemba 26, 2026, kuadhimisha sikukuu ya utoaji shukrani au Thanksgiving, inayosherehekewa nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ubalozi huo, huduma zote za kawaida za kibalozi zimesitishwa kwa siku ya leo.

Huduma zilizoathiriwa ni pamoja na mahojiano ya visa, uhuishaji wa pasipoti na huduma za uthibitishaji wa nyaraka.

Mawasiliano ya kawaida kupitia simu na barua pepe pia yamesitishwa, ingawa waombaji bado wanaweza kujaza fomu mpya za maombi ya visa na kulipa ada kupitia mtandao.

Hata hivyo, ubalozi huo umethibitisha kuwa huduma za dharura kwa raia wa Marekani wanaoishi nchini Kenya au wanaosafiri nchini humo zitaendelea kupatikana kupitia mifumo yake ya usaidizi wa dharura nje ya saa za kawaida za kazi.

Huduma za kawaida katika ubalozi huo zinatarajiwa kurejea kesho, Ijumaa, Novemba 27, 2026.

Share This Article