Majaribio ya kitaifa ya siku tatu kuchagua timu za Kenya zitakazoshiriki mashindano ya Afrika nchini Ghana, na mbio za Dunia za kupokezana kijiti nchini Botswana yameanza leo katika uwanja wa Ulinzi.
Majaribio hayo yanawaleta pamoja wanariadha zaidi ya 800, walioalikwa na chama cha Riadha Kenya.
Mbio za Dunia za kupokezana kijiti mjini Gaborone, Botswana kati ya tarehe 2 na 3 mwezi ujao,huku makala ya 24 ya mashindano ya Riadha Afrika yakifanyika nchini Ghana kuanzia Mei 12 hadi 17.