Magari ya kwanza ya umeme laki moja kutotozwa ushuru

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto ametoa wito kwa Wakenya kukumbatia matumizi ya magari ya umeme kama suluhu kwa changamoto za usambazaji wa mafuta nchini wakati wa majanga. 

Amesema tayari serikali imekumbatia matumizi ya magari hayo.

“Serikali tayari imeagiza magari ya umeme 3,000 kupitia Wizara ya Usalama wa Taifa ili kutumiwa na maafisa wa usalama na utawala,” alisema Rais Ruto wakati bei za mafuta nchini zikipanda kutokana na mgogoro wa Mashariki ya Kati.

“Pia natoa tangazo kwamba magari ya kwanza ya umeme 100,000 kuagizwa nchini Kenya, ama kwa ajili ya matumizi ya umma au binafsi, hayatatozwa ushuru hata wakati tukiendelea kufanya kazi na sekta ya kibinafsi kwa wawekezaji katika utengenezaji wa magari ya umeme kuanzisha vituo vya uzalishaji nchini Kenya.”

Tangazo hilo huenda likachochea uagizaji wa magari ya umeme katika nchi ambayo idadi ndogo ya watu wamekumbatia magari hayo.

 

Share This Article