Maambukizi 12,000 ya Ebola yamenakiliwa nchini DRC

Maafisa wa afya wanaokabiliana na ugonjwa huo, wamelazimika kuondoka katika maeneo yaliyo na ghasia wakihofia usalama wao.

Tom Mathinji
1 Min Read
Maambukizi 12,000 ya Ebola yamenakiliwa nchini DRC.

Visa vya ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), vimedizi 12,000, kulingana na takwimu za serikali ya nchi hiyo.

Mapigano yanayoshuhudiwa mashariki ya DRC, yanatatiza juhudi za kukabiliana na msambao wa ugonjwa huo ambao chamko lake limetajwa kuwa hatari zaidi katika historia ya taifa hilo.

Maafisa wa afya wanaokabiliana na ugonjwa huo, wamelazimika kuondoka katika maeneo yaliyo na ghasia wakihofia usalama wao.

Mapigano katika mkoa wa Ituri yameongezeka katika siku za hivi karibuni kati ya majeshi ya DRC na wapiganaji wa kundi la CRP, huku wakazi wakilazimika kutoroka, kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa.

Catherine Smallwood, msimamizi Shirika la Umoja wa Mataifa dhidi ya Ebola, alisema wakazi, maafisa wa afya na maafisa wa WHO walihamishwa hadi katika eneo la Bunia, baada ya kujificha katika hospitali ya Akwe kutokana na mapigano hayo.

“Walijipata katikati ya mapigano, lakini tulifanikiwa kuwaokoa,” alisema Smallwood.

Serikali ya DRC imenakili maambukizi 12,021 ya Ebola na vifo 5,904 kutokana na makali ya ugonjwa huo.

TAGGED:
Share This Article