Maafisa wa serikali ya Uganda wakamatwa kwa udukuzi

BBC
By
BBC
1 Min Read

Polisi nchini Uganda wanawashikilia maafisa tisa wa Wizara ya Fedha kama sehemu ya uchunguzi wa tuhuma za kudukua mifumo ya kielektroniki ya benki kuu na kusababisha wizi wa shilingi bilioni 62 (dola milioni 16.87), imesema wizara na polisi.

Mwezi Novemba mwaka jana, Waziri wa Fedha Henry Musasizi alithibitisha kwa vyombo vya habari vya nchi hiyo kwamba akaunti za benki kuu zilidukuliwa na pesa kuibiwa.

Polisi na Wizara ya Fedha wanasema wanaozuiliwa ni pamoja na afisa mkuu wa idara ya hazina ya Wizara hiyo.

Baadhi ya maafisa kutoka ofisi ya mhasibu mkuu katika wizara hiyo “waliitwa na kushikiliwa ili kuwezesha uchunguzi,” wizara ya fedha ilisema kwenye chapisho kwenye akaunti yake ya X jana Jumanne jioni.

Wizara haikutoa majina ya waliozuiliwa wala idadi yao.

Hata hivyo, msemaji wa polisi Kituuma Rusoke, aliambia televisheni ya NTV kuwa maafisa tisa wamezuiliwa na kusoma majina yao.

Gazeti la serikali la New Vision liliripoti kwamba wadukuzi, wakijitambulisha kama “Taka”, walidukua mifumo ya IT ya Benki ya Uganda na kuhamisha fedha hizo kinyume cha sheria.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *