Ligi Kuu Kenya kung’oa nanga Septemba 19

Jaji wa Mahakama kuu ya Murang'a Dorah Chepkwony aliamrisha kuanza kwa Ligi kwa kutumia mfumo wa mwaka 2019.

Dismas Otuke
1 Min Read
Gor Mahia FC Crowned FKFPL Champions 2025/2026

Shirikisho la kandanda nchini Kenya (FKF) limatangaza kuanza rasmi kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya wanaume wa mwaka 2026/2027,Septemba 19 kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama wa Agosti 28.

FKF imezitaka timu kujiandaa kwa msimu mpya na pia kuwataka mashabiki kushabikia vlabu vyao.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Waziri wa Michezo kukutana na wenyeviti wa timu zote 16 zinazopaswa kushiriki Ligi hiyo na kuwataka wenyeviti hao kuweka kando maslahi yao na kuruhusu ligi kuanza.

Klabu ya Kariobangi Sharks ilikuwa imeenda mahakamani kupinga kuenguliwa ligini huku ikipinga mfumo uliotumika.

Jaji wa Mahakama kuu ya Murang’a Dorah Chepkwony aliamrisha kuanza kwa Ligi kwa kutumia mfumo wa mwaka 2019.

Share This Article