Kuna akiba ya kutosha ya mafuta, Waziri Wandayi awahakikishia Wakenya

Hofu imetanda kuwa bei za mafuta huenda zikapanda kutokana na mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati ambao umesababisha uhaba wa bidhaa hiyo duniani.

Martin Mwanje
1 Min Read
Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi akiwahutubia wakazi wa wadi ya Tendeno-Sorget, eneo bunge la Kipkelion Mashariki

Serikali imewahakikishia Wakenya kwamba kuna akiba ya kutosha ya mafuta nchini. 

Hakikisho hilo linakuja wakati ambapo kuna hofu kwamba bei za bidhaa hiyo muhimu huenda zikapanda serikali itakapotangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu.

Bei hizo zinatarajiwa kutangazwa kesho Jumamosi.

Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi anasema serikali inafanya kazi na kampuni tatu za kimataifa kuhakikisha hakutakuwa na uhaba wa mafuta nchini.

Hata hivyo, hakusema Kenya ina kiasi gani cha mafuta na yanaweza yakadumu kwa kipindi gani.

Waziri Opiyo alitoa hakikisho hilo wakati wa uzinduzi wa miradi ya usambazaji umeme mashinani uliofanyika katika wadi ya Tendeno-Sorget, eneo bunge la Kipkelion Mashariki, kaunti ya Kericho.

Matamshi yake yanakuja wakati ambapo bei za mafuta zimeripotiwa kupanda duniani kutokana na mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati.

Chanzo cha mgogoro huo ni hatua ya nchi za Marekani na Israel kuishambulia Iran.

Kiongozi Mkuu mpya wa Iran

Inahofiwa kwamba Mojtaba Khamenei ameapa kulipiza kisasi.

Inahofiwa kwamba tangazo la Khamenei kwamba Mlango Bahari wa Hormuz utaendelea kufungwa ili kumshinikiza adui huenda likaharibu mambo zaidi.

Taarifa hii imechangiwa na mwandishi wetu Erick Kiplangat

 

 

Share This Article