Kombe la Dunia laingia siku ya 15 huku makundi ya D, E na F yakihitimisha mechi

Mataifa mengine yaliyojikatia tiketi kwa awamu hiyo ya 32 bora ni Ujerumani, Argentina, Ufaransa, Bosnia Hezgovina na Afrika Kusini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia zitaingia siku ya 15 kwa mechi za mwisho za makundi ya D, E na F. 

Timu 13 zimefuzu kwa hatua ya 32 bora zikiwa Norway, Colombia, Uswizi, Brazil, Morocco, Marekani, Canada na Mexico.

Mataifa mengine yaliyojikatia tiketi kwa awamu hiyo ya 32 bora ni Ujerumani, Argentina, Ufaransa, Bosnia Hezgovina na Afrika Kusini.

Curacao watafungua ratiba ya kundi E, Alhamisi saa tano usiku dhidi ya Ivory Coast  katika uwanja wa Philadelphia nchini Marekamni, mshindi akifuzu kwa raundi ya 32 bora.

Ujerumani waliojihakikishia nafasi ya kwanza kundini humo huenda wakawapumzisha wachezaji wao wa kikosi cha kwanza watakapopimana nguvu na Ecuador katika uga wa New York, New Jersey pia saa tano.

Baadaye saa nane usiku, kivumbi kinatarajiwa kundi F Japani wakishuka uwanjani dhidi Uswidi katika kiwara cha Dallas huku Uholanzi wakikabiliana na Tunisia ugani Kansas City.

Waandalizi wenza Marekani ambao tayari wamejihakikishia nafasi ya kwanza watakuwa kiwarani Los Angeles kuanzia saa kumi na moja ashubuhi Ijumaa dhidi ya Uturuki katika kundi D, kisha Australia na Paraguay walio na alama sawa tatu, wapambane  katika uchanjaa wa Samn Francisco Bay Area saa kumi na moja.

Share This Article